Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Bani Israil 17:25

17:25
ربكم اعلم بما في نفوسكم ان تكونوا صالحين فانه كان للاوابين غفورا ٢٥
رَّبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَا فِى نُفُوسِكُمْ ۚ إِن تَكُونُوا۟ صَـٰلِحِينَ فَإِنَّهُۥ كَانَ لِلْأَوَّٰبِينَ غَفُورًۭا ٢٥
رَّبُّكُمۡ
أَعۡلَمُ
بِمَا
فِي
نُفُوسِكُمۡۚ
إِن
تَكُونُواْ
صَٰلِحِينَ
فَإِنَّهُۥ
كَانَ
لِلۡأَوَّٰبِينَ
غَفُورٗا
٢٥
Mola wenu anajua kabisa yaliyo nyoyoni mwenu. Ikiwa nyinyi mtakuwa wema, basi hakika Yeye ni Mwenye kuwaghufiria wanao tubia kwake. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mola wenu, enyi watu, ni Mjuzi zaidi wa mazuri na mabaya yaliyomo ndani ya nyoyo zenu. Iwapo matakwa yenu na makusudio yenu ni kumridhisha Mwenyezi Mungu na kujikaribisha Kwake, basi Yeye, kutakata na sifa mbaya ni Kwake, kwa wenye kurejea Kwake katika nyakati zote ni Mwingi wa kusamehe. Basi yoyote yule ambaye Mwenyezi Mungu Amejua kwamba hakuna katika moyo wake isipokuwa ni kurejea Kwake na kumpenda, Yeye Atamsamehe na Atamghufiria yatakayotukia miongoni mwa madhambi madogo yanayolingana na tabia za kibinadamu.